Kampuni ya Ndanda Pure spring water ya mkoani Mtwara imefungiwa kwa muda
usiojulikana. Hii ni kutokana na kubainika kuwa maji yake yaliyopo
sokoni hivi sasa ni machafu. Akiongea na radio Pride FM ya mjini hapa, afisa
afya wa mkoa amesema sampo ya maji hayo imepelekwa Dsm mamlaka ya chakula
na dawa ili yafanyiwe uchunguzi kuona kama uchafu huo una athari zipi kwa
mlaji na kwamba tayari ameshapeleka barua kwenye kampuni hiyo kusimamisha
shughuli za kiwanda hicho.
Source: Amka Na Pride Fm