LICHA ya mwaka jana kuita vyombo vya habari na kujisafisha baada ya kukaa nusu utupu jukwaani, mastaa wawili wa filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu na Aunt Ezekiel wamefanya uchafu wakiwa Hong Kong, China.
Video ya aibu ya wawili hao ilivuja mitandaoni mwishoni mwa wiki iliyopita ikiwaonesha ‘wakidendeka’ na kufanyiana vitendo vinavyokwenda kinyume na maadili ya Kitanzania.
Katika video hiyo waliyorekodi wakiwa China, wawili hao wanaonekana kwenye chumba wakiimba wimbo wa ‘Happy Birthday’ na baada ya kumaliza, wakasogezeana midomo na kumwagiana mabusu ya nguvu.
Kwa mujibu wa mashabiki wao walioiona video hiyo, wasanii hao wanatakiwa kutambua kwamba wao ni kioo cha jamii huku Aunt akipondwa zaidi kwa kuwa ni mke wa mtu, Sunday Demonte.