MASTAA: TUMEJIPANGA HARAMBEE YA KUDHIBITI KANSA KWA WANAWAKE


Mkurugenzi wa Utafiti na Udhibiti Kansa, Dk. Julius Mwaiselage.

NA JELARD LUCAS
BAADHI ya mastaa wa sinema za Kibongo wameweka 'plain' kuwa wako bega kwa bega kuunga mkono harambee ya kusaidia udhibiti wa kansa ya matiti kwa wanawake nchini inayoendeshwa na taasisi ya kudhibiti kansa (Ocean Road Cancer Institute ‘ORCI’)  iliyo chini ya Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam.

Harembee hiyo inatarajiwa kufanyika Oktoba  12 mwaka huu katika hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar.
Hata hivyo malengo ya harambee hiyo ni kupata kiasi cha shilingi milioni 32 za Kitanzania ili kusaidia wanawake wanaosumbuliwa na kansa ya matiti nchini.

Mastaa wa sinema za Kibongo wamepewa kipaumbele katika kufanikisha zoezi hilo na wageni wengine 84 kuhudhuria harambee hiyo.
Hawa ni baadhi tu ya mastaa wa sinema za Kibongo ambao wameongea na mwandishi wetu juu ya harabee hiyo:
Steven Mangere ‘Steve Nyerere’
“Niko tayari kuhudhuria harambee hiyo na nimefurahi kuchaguliwa kuwa balozi juu ya tukio hili, naomba mastaa wenzangu wajitokeze ili kuinua afya ya mwanamke nchini, taifa letu bila mwanamke haliwezi kusonga mbele naomba tuwaunge mkono”alisema Steve.

Nargis Mohammed
“Najipanga kuimarisha jitihada ya utu mwanamke, nimefurahi sana kupewa heshima hiyo kwani niko tayari, taarifa hizo zipo nimezisikia japo sijapata barua rasmi, niko bega kwa bega kwani sisi wanawake inatuhusu moja kwa moja na sina pingamizi juu ya hilo” alisema Nargis.

Batuli ‘Yobnesh Yusuf’
“Nimepigiwa simu na mheshimiwa mmoja juu ya hilo, niko tayari japo sijapata mwaliko 'official' lakini tayari nimejipanga kukabiliana na hilo juu ya utekelezaji wa maisha ya mwanamke, kansa ya matiti ni zaidi ya Ukimwi, mtu yeyote aliyepewa mwaliko akipuuza nitamshangaa, binafsi niko tayari na nimejipanga vilivyo” alisema Batuli akiwa maeneo ya Kigamboni.

Jacob Steven ‘JB’
“Niko nje ya mji, bado sijapokea mwaliko huo nikipata nitaufanyia kazi maana wewe ndiyo unanipa taarifa hizo lakini ni kitu kizuri na niko tayari”
Kauli mbiu ya harambee hiyo ni ‘With Heart & Desire We Can Have a Breast Cancer Free in Tanzania’ ikiwa na maana ‘Kwa Moyo na Nia Tunaweza Kutokomeza Kansa ya Matiti Tanzania’ shughuli yote inaendeshwa chini ya Mkurugenzi wa Utafiti na Udhibiti Kansa, Dk. Julius Mwaiselage.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...