WAZIRI KAGASHEKI AONGOZA MATEMBEZI YA SIKU YA TEMBO DUNIANI JIJINI ARUSHA LEO


 Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki akikata utepe kuashiria uzinduzi wa matembezi ya amani ya Tembo Duniani kupinga mauaji ya tembo.
 Waziri Kagasheki akionesha moja ya vibao ambavyo vinawaonesha tembo wakati wa matembezi hayo ya amani.
 Kutoka kushoto ni Mrs. Tibaijuka akifuatiwa na Waziri Kagasheki, Mwenyekiti wa Tanzania Association of Tours Operators Willbert Chambulo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Magesa Mulongo.
 Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika matembezi ya Siku ya Tembo Duniani.
 Baadhi ya wanaharakati wakiwa katika matembezi ya siku ya Tembo Duniani.
 Maelfu ya wananchi kutoka Arusha pamoja na wadau wengine kutoka mikoa na nchi mbalimbali wakiwa katika matembezi ya siku ya Tembo Duniani yaliyofanyika Arusha leo.
 Hawa ni watoto shupavu kabisa waliojitokeza mstari wa mbele katika matembezi ya Tembo leo.
  Waziri Kagasheki akisaini katika moja la bango la siku ya Tembo, ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu.
 Maandamano yakiendelea.
 Wa kwanza kutoka kulia ni Bw. Peter ambaye ndiye alikuwa katika kamati kuu ya maandalizi ya matembezi ya Siku ya Tembo Duniani na pia makamu mwenyekiti wa Tanzania Association of Tours Operators akiwa katika matembezi hayo.
  Waziri Kagasheki akiongoza maelfu ya watu kuingia katika Viwanja vya AICC ambapo ndipo ilikuwa kilele cha matembezi hayo.
 Afisa Mtendaji wa Chama cha Wakala wa Utalii TATO, Sirili Akko akitoa maneno machache kabla ya ufunguzi rasmi wa kilele cha matembezi ya Tembo Duniani.
 Meza kuu wakiongozwa na Waziri Kagasheki (wa nne kutoka kushoto) wakiwa wamesimama kwa muda wa dakika moja kuwakumbuka waliokufa katika tukio la kigaidi la Westgate, nchini Kenya pamoja na tembo wote waliouwawa mpaka sasa.
 Mc akiwakaribisha viongozi mbalimbali kwa ajili ya kutoa salamu zao.
 Dk. Alfred Kikoti akitoa mada yake juu ya idadi ya tembo waliopo hivi sasa.
Mwenyekiti wa Tanzania Association of Tours Operators, Wilbert Chambulo akielezea juu ya kusimamisha biashara kubwa ya meno ya tembo ambayo inaongozwa na nchi ya China na kuziomba nchi nyingine kusimamisha biashara hiyo haramu.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akiwashukuru wananchi wa Arusha kwa kushiriki kikamilifu zoezi la matembezi ya Siku ya Tembo Duniani na kumkaribisha Mgeni Rasmi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki  kutoa hotuba yake.
Waziri Kagasheki akizungumza na wanaharakati waliofika katika matembezi ya Siku ya Tembo Duniani, kwa kutoa salamu kutoka kwa Mheshimiwa Rais Kikwete kwamba oparesheni ya kutokomeza majangili imeanza na haitasimama, alisisitiza kwamba wanasheria wafunge midomo yao kuhusu kutetea haki za binadamu, aliongeza kwamba majangili wauawe huko huko wakikamatwa kurahisisha msongamano wa kesi mahakamani na mwisho aliongeza kwamba wanasiasa wasiingilie suala hili la kupambana na ujangili.
Waziri Kagasheki akikabidhi vyeti kwa shule zilizoshiriki katika matembezi hayo.
 Waziri Kagasheki akipokea zawadi kutoka kwa TATO, anayemkabidhi zawadi hiyo ni Makamu Mwenyekiti wa TATO, Peter.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akipokea zawadi kutoka TATO, anayemkabidhi ni Bi. Tibaijuka.
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa, Allan Kijazi akitoa neno la shukurani wakati wa kufunga kilele cha siku ya matembezi ya tembo.
Hawa ni wale waliotembea katika matembezi ya kupinga mauaji ya tembo kutoka Arusha hadi Dar es Salaam Mwendo wa Kilometa 650 kwa siku 12. Kutoka kushoto ni binti mdogo mwenye umri wa miaka 20 Kaptorina Manange, Mkazeni Y. Mkazeni, Rehema Y. Najema na Livingstone Y. Mkazeni. 
(Picha zote na Blogs za Mikoa)


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...