Watu saba wamepoteza maisha katika ajali huyo akiwemo dereva wa Noah aliyejulikana kwa jina la Masoud Juma na wengine wanne hali zao ni mbaya. "Chanzo cha ajali hii ni dereva wa Noah ambaye alikuwa akijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake na ghafla akakutana na lori uso kwa uso" Alisema Bw. Sanjo Ole ambaye ni mfugaji jamii ya Kimasai.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile amedhibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
(HABARI NA DUSTAN SHEKIDELE / GPL, MOROGORO)
(HABARI NA DUSTAN SHEKIDELE / GPL, MOROGORO)