BREAKING NEWS: RAGE ASIMAMISHWA SIMBA, KIBADENI, JULIO WATIMULIWA SIMBA



Ismail Aden Rage.
Kamati ya utendaji ya klabu ya Simba iliyokutana jana usiku, imemsimamisha kazi Mwenyekiti Ismail Aden Rage.
Rage amesimamishwa kazi kutokana na masuala kadhaa, lakini kubwa imeelezwa ni suala la mauzo ya mchezaji Emmanuel Okwi.


Julio(kulia) na Kibadeni(kushoto) wameondolewa kazini.

Julio na Kibadeni wameondolewa kazini baada ya kamati ya utendaji iliyokutana jana kufikia uamuzi kwamba wawili hao utendaji wao si sahihi.Tayari Simba imekamilisha mazungumzo na kocha mwingine mzungu, si yule Bobby Willliamson ambaye aliandikwa na gazeti moja nchini kwamba ndiye kocha mpya wa Simba.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...