Waziri
wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akizungumza na watendaji
wa shirika la umeme nchini (Tanesco) ikiwa ni pamoja na wadau wa umeme
mjini Morogoro kabla ya kuanza rasmi ziara yake kwenye miradi ya umeme.
Waziri
wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akitoa maelekezo kwa meneja
wa Tanesco mkoa wa Morogoro Deogratius Ndamugoba mara baada ya kujionea
moja ya transfoma iliyojengwa kwa ajili ya kupeleka umeme katika kijiji
cha Matombo kilichopo katika wilaya ya Morogoro Vijijini.
Kazi
ya kuweka umeme ikiwa ni pamoja na kufunga mita ikiendelea kwenye moja
ya nyumba zilizopo katika kijiji cha Mtombozi kilichopo katika wilaya ya
Morogoro Vijijini.
Waziri
wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akizungumza na wakazi wa
kijiji cha Mtombozi kilichopo katika wilaya ya Morogoro Vijijini wakati
wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi ya umeme.
Meneja
wa Tanesco mkoa wa Morogoro Deogratius Ndamugoba akitoa ufafanuzi wa
maendeleo ya miradi ya umeme katika kijiji cha Mtombozi mbele ya Waziri
wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo.
Waziri
wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akisalimiana na mmoja wa
wakazi wa kijiji cha Ngong’oro kabla ya kusikiliza kero zao ikiwa ni
pamoja na kuzungumza nao
Mwenyekiti
wa kijiji cha Ngong’oro Mahamba Shukuru akiwasilisha changamoto katika
upatikanaji wa huduma ya umeme katika kijiji hicho kwa Waziri wa
Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo ambapo Waziri huyo ameahidi
kufanyia kazi mara moja kupitia kwa watendaji wake.