KESI YA KUKUTWA NA SIMU GEREZANI:.LIYUMBA ATINGA MAHAKAMANI

Mabaunsa wakimkinga Liyumba.

Juhudi za kumkinga zikiendelea.
Akikimbizwa kuwakwepa mapaparazi.  
 ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Miradi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba, leo alitinga katika mahakama ya Kisutu kusikiliza kesi yake akiwa na kundi la mabaunsa waliokuwa wakimkinga asipigwe picha na mapaparazi. Liyumba alitinga mahakamani hapo kusikiliza kesi inayomkabili ya kunaswa na simu ya kiganjani akiwa gerezani ambapo leo ilikuwa siku ya kumsikiliza shahidi wa upande wa mashitaka lakini shahidi huyo alipatwa na udhuru hivyo kesi hiyo kuahirishwa mpaka Novemba 26 mwaka huu.
                                                               PICHA : RICHARD BUKOS / GPL


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...