Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Mh. January Makamba.
· Wakali watano Ligi kuu ya Vodacom kuchuana
· Amri Kiemba, Haruna Niyonzima, Shomari Kapombe, Themi Felix, Na Kelvin Yondani.
Dar es Salaam, 6th Nov 2013. Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Mh. January Makamba anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa tuzo kwa mwana soka bora wa mwaka katika ligi kuu ya Vodacom mwaka 2013, itakayofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Tuzo hiyo itashuhudia wachezaji walioingia hatua ya Tano bora, AMRI KIEMBA, HARUNA NIYONZIMA, SHOMARI KAPOMBE, THEMI FELIX, na KELVIN YONDANI wakichuana kuwania umwamba wa soka Tanzania, Baada ya kupigiwa kura na mashabiki na Kamati maalum chini ya Mwenyekiti wake Zamoyoni Mogela kuchambua majina hayo kulingana na kura walizopata.
Akizungumza juu ya hafla hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Kelvin Twissa amesema, wanafurahi kuwa sehemu ya maendeleo ya soka nchini na siku zote kampuni yake imekuwa msitari wa mbele katika kuunga mkono michezo nchini, hususani mchezo wa soka na kuhakikisha unakuwa moja ya ajira muhimu kwa watanzania.
“Vodacom tumeendelea kuwa wadau muhimu katika mapinduzi ya soka la Tanzania, sasa mpira umekuwa zaidi ya burudani kwa watanzania kutokana na chachu ambayo tumeiweka tangu tuanze kudhamini ligi kuu, ambayo sasa imekuwa na ushindani mkubwa na thamani yake inazididi kupanda siku hadi siku,” alisema Twissa.
Aidha Twissa amesema kampuni yake itaendelea kushirikiana na wadau wengine wote wanaopenda maendeleo ya soka bila kusita kutokana na namna ambavyo kampuni yake imejidhatiti katika kuinua michezo nchini.
“Mafanikio yanayopatikana katika soka letu sasa hayajapatikana hivivi ni kutokana na dhamira tuliyoiweka katika kuinua mchezo huu wa soka na uwekezaji mkubwa tulioufanya hadi sasa, watu ambao wanaleta mafanikio haya ni wachezaji ambao wamekuwa wanapambana kufa na kupona kutoa burudani kwa Watanzania, Ni lazima tuwaenzi wachezaji hawa kwa njia tofauti tofauti,” alisema Twissa.
Kwa upande wake Meneja Masoko wa MCL Bernad Mukasa amesema kuwa, wamefurahi kushirikiana na Naibu waziri Mh. Makamba katika utoaji wa tuzo hizi, ambazo zinatambua mchango wa wanasoka nchini.
“Tuzo hizi zinatambulika rasmi kwa jina la zitaitwa MWANASPOTI BORA WA SOKA WA VODACOM 2013. Ni za kipekee na za kwanza kabisa nchini kwa wigo wa wachezaji wanaohusishwa, ushirikishwaji wa uteuzi wa mshindi, na vigezo husika.” alisema Mukasa na kuongeza.
“Kwa mwaka huu, licha ya kumpata Mwanaspoti Bora wa soka wa mwaka , pia tutatoa Tuzo kwa “categories” zaidi ya 10 ikiwemo kocha bora, mwamuzi bora, mchezaji bora wa kike, mchezaji bora chipukizi, “1st eleven”, goli bora, mchezaji bora wa kigeni, Mchezi bora wa kulipwa anayecheza nje, na Kipengele kingine kitajulikana siku ya ijumaa.” Alisema Mukasa.
Mukasa alihitimisha kwa kutoa wito kwa Watanzania kuendelea kuwapigia kura wachezaji hao kwa kuandika ujumbe mfupi unaoanza na neno KURA kisha jina la mchezaji anayemchagua kati ya hao waliotajwa na kisha kutuma kwenda namba 15678.