TASWIRA ZA MISS UNIVERSE 2013 MJINI MOSCOW, URUSI

Miss Universe 2013, Gabriella Isler (25) akiwapungia mashabiki baada ya kutwaa taji hilo mjini Moscow, Urusi usiku wa kuamkia leo.
Miss Universe 2012, Olivia Culpo kutoka Marekani, akimvisha taji la Miss Universe 2013, Gabriella Isler wa Venezuela usiku wa kuamkia leo mjini Moscow, Urusi.
Miss Universe 2013, Gabriella Isler akipozi kwa picha wakati wa mkutano na wanahabari kwenye Ukumbi wa Crocus City mjini Moscow, Urusi usiku wa kuamkia leo.
Washiriki 86 wa shindano la Miss Universe 2013 wakiwa katika pozi kwenye Ukumbi wa Crocus City mjini Moscow, Urusi usiku wa kuamkia leo.
MISS Venezuela Gabriella Isler (25), ametwaa taji la Miss Universe 2013 usiku wa kuamkia leo mjini Moscow, Urusi. Gabriella aliwabwaga washiriki wenzake 85 kutoka mataifa tofauti waliokuwa wanashindania taji hilo. Walioingia Top 5 ni Miss Ecuador, Miss Brazil, Miss Venezuela, Miss Philippines na Miss Spain. Nafasi ya pili katika kinyang'anyiro hicho ilikwenda kwa Miss Spain Patricia Yurena Rodriguez na Mshindi wa tatu alikuwa Miss Ecuador Constanza Baez.
(PICHA ZOTE: AFP)


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...