WAWEKEZAJI KUTOKA UBELIGIJI WAWASILI TANZANIA KUANGALIA FURSA ZA UWEKEZAJI‏

1
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Dk. Diodorus Kamala akiwakaribisha miongoni mwa wawekezaji 65 kutoka taasisi ya Flanders Investiment & Trade ya nchini Ubeligiji waliowasili jana mchana kwa ndege ya shirika la ndege la Kenya Airways kwa ajili ya kuja kuangalia fursa za uwekezaji nchini Tanzania wawekezaji hao wamekuja nchini kwa juhudi kubwa za balozi Dk. Diodorus Kamala anazofanya nchini humo kama mwakilishi rasmi wa nchi ya Tanzania.
3
 Dk. Kamala akiongozana na kiongozi wa wawekezaji hao Bw. Malin. Kulia ni Bw Hassan mmoja wa waratibu wa ujio wa wawekezaji hao.
4
 Dk. Kamala akiwaongoza wekezaji hao ambao watakuwa na mkutano wawekezaji wa hapa nchini pia.
5
Wawekezaji hao wakisubiri usafiri tayari kwa kuelekea kwenye hoteli ya Serena Dar es Salaam.
6
Dk. Kamala akifafanua jambo kwa wawekezaji hao.
7
Dk. Kamala akihojiwa na waandishi wa habari kutoka kituo cha ITV ambao walifika katika mapokezi hayo.

(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE- JKN AIRPORT)


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...