Home »
Uncategories »
TIGO REACH FOR CHANGE KUWASAIDIA WATOTO NCHINI TANZANIA
TIGO REACH FOR CHANGE KUWASAIDIA WATOTO NCHINI TANZANIA
Unknown
1:16 PM
Mkurugenzi
Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez, akizungumza na Waandishi wa
Habari katika uzinduzi wa programu maalum ya ‘Reach for Change’ ambapo
watanzania watatu wenye wazo bora yakuwasaidia watoto watapata fursa
yakujishindia dola 25,000 kila mwaka kwa muda wa miaka mitatu ili
kuendesha miradi yao.
Meneja
Huduma kwa Jamii wa Tigo Bi. Woinde Shisael akitoa maelezo zaidi kuhusu
programu maalum ya ‘Reach for Change’ inayowawezesha wajasirialamali
jamii kutekeleza miradi yao yakuwasaidia watoto.
Waandishi
wa Habari wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tigo
Tanzania, Diego Gutierrez, aliyesisitiza Watanzania kujitokeza kwa wingi
kuandika miradi ambayo yatalenga kupata haki na kuinua ubora wa maisha
ya watoto nchini.
Mkurugenzi
Mkazi wa shirika la Reach for Change nchini Tanzania na Rwanda, Richard
Gorvett, akizungumza na Waandishi wa Habari. Katikati ni Mkurugenzi
Mkuu wa Tigo Tanzania, Diego Gutierrez, akifuatiwa na Meneja Huduma kwa
Jamii wa Tigo Bi. Woinde Shisael.