Diamond Platnumz kuwasomesha watoto watatu walioshinda shindano la kucheza Ngololo

Diamond Platnumz ni bingwa wa kuitumia karata yake ya Public Relations vizuri. Mwezi August mwaka huu aliicheza vizuri  baada ya kumfanyia surprise mwanamuziki mkongwe wa Tanzania Muhidin Gurumo kwa kumnunulia gari kwenye uzinduzi wa video yake ya 'My Number One' uliofanyika Serena Hotel jijini Dar es Salaam.
Jumatano hii, staa huyo aliyekuwa ameandaa show maalum ya Christmas kwaajili ya watoto kwenye viwanja vya Leaders Club, alitisha tena baada ya kuahidi kuwasomesha bure watoto watatu walioshinda shindano la kucheza mtindo wake wa Ngololo.
"Management yangu ya WCB itawasomesha miaka yote waliyobakiza shuleni ikiwa ni pamoja na kuwahamishia katika shule zilizo bora zaidi,"aliandika Diamond kwenye website yake.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...