Khadija Kopa |
MALKIA
wa Mipasho Bongo, Khadija Omar Kopa amefunguka kuwa, tangu atoke eda
amekuwa akisumbuliwa na wanaume wengi wakitaka kumuoa licha ya yeye
kutokuwa na mawazo hayo kwa sasa.
Akizungumza
hivi karibuni jijini Dar, Khadija alisema kiukweli mawazo ya kumtafuta
mrithi wa marehemu mume wake, Jafari Ally, hayapo kwa sasa ila amekuwa
akipokea simu nyingi na meseji kibao za wanaume wanaoomba nafasi.
“Kwa
kweli sina mawazo ya kuolewa kwa sasa lakini ni kweli nimekuwa nikipata
usumbufu mkubwa sana kutokwa kwa wanaume wanaotaka ndoa na mimi.
“Siwezi
kusema sitaolewa milele kwani Mungu ana mipango yake ila mara nyingi
ninapofikiria kuolewa tena nahisi mwanaume nitakayempata anaweza
kuniumiza na kunifanya nimkumbuke marehemu mume wangu,” alisema Khadija
Kopa.