MALORI YAGONGANA NA KUZIBA NJIA ENEO LA WAMI, MSAADA UNAHITAJIKA‏

 Malori yaliyogongana yakiwa yameziba njia baada ya kugongana eneo la Mto Wami.
 Foleni ni kubwa sana ya mabasi yaendayo mikoa ya Tanga, Arusha na Kilimanjaro.
Ajali mbaya imetokea muda huu eneo la Mto Wami na kusababisha foleni kubwa sana kwa magari na mabasi yanayotumia njia hiyo, Dj sek blog imefanikiwa kupata picha kadhaa za ajali hiyo. Chanzo cha ajali inadaiwa ni kufeli breki kwa malori hayo yakiwa yanateremka kwenye mlima huo. Polisi wanaendelea na jitihada za kuyatoa ili njia ipatikane kwa ukubwa zaidi ili kuruhusu upitaji mzuri wa magari.

PICHA NA HABARI KWA HISANI YA DJ SEK BLOG


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...