SNURA AWASHUKURU WALIOMTOA, WEMA SEPETU, TUNDAMAN, MAREHEMU SHARO WATAJWA

Snura Mushi.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii mwanadada Snura mushi alimua kufunguka yafuatao kwa mdada Wema Sepetu, Tundaman, Chekibudi na Marehemu Sharo Milionea kwa jinsi walivumsaidia kufika hapo alipo leo. Snura alisema yafuatayo…
Kwa Wema Sepetu
Msema kweli mpenzi wa mungu wakati narecod wimbo wangu wa kwanza wema alihusika sana...hela yake ilihusika studio, sauti yake ilihusika kwenye wimbo huo ambao ni shogaake mama ...vazi langu la show kwa mara ya kwanza wema ndio alinibunia namm nimeliandeleza vazi hilo mpaka leo kwenye show zangu sina chakukulipa wema ila nakushukuru sana nakuombea kwa mungu akubariki zaidi na zaidi wema sepetu...

Kwa Tundaman
Sijui nianzie wapi lakini huyu ndio mtu alie tumia nguvu kuniingiza kwenye muziki baada ya kuona kama siwaelewi hivi kila waliponiambia ....wakati anazindua album yake ya starehe gharama pale maisha aliamua kutengeneza tangazo ambalo lilisema snura atatambulisha wimbo wake mpya kwa mara ya kwanza kiukweli alinivuruga kwasababu mm sikua na wimbo wowote sasa kwa kuhofia aibu nishatangazwa ndio nikalazimika kwenda kurecod shogaake mama haraka sana na nikafanya hiyo show watu wakanielewa sana huo ndio ulikua mwanzo ....leo hii nimeona faida yake asante sana kakaangu tunda man mungu akubariki sana umekua mtu muhim sana kwenye maisha yangu tuendelee kushikana hivihivi kwa shida na raha nakupenda sana kakaangu  tunda man captain ...msambinungwa..

Kwa Chekibudi
Ningependa kuanza na movie kabla ya muziki...japokua mwaka huu nimefanya vizuri sana katika muziki...basi kama kuna mtayarishaji wa movie anae tambua na kuthamini kipaji changu ni huyu ....nakushukuru sana kakaangu chekbud kwa kutambua umuhim wangu asante sana kaka ....nadhani kama ww nimshabiki wangu kwenye movie utakubaliana na hilo hakuna movie ya chekibudi mimi sipo...nakutakia kila lakheri brother. ....shukrani zinaendelea fuatilia ujue nani anafuata wako wengu kuna vitu vingi sana mtavijua ambavyo naamini hamjawahi kuvisikia mtavijua kupitia mtiririko huu wa shukrani.....

Kwa marehemu Sharo Milionea
Alinipigia kelele sana nifanye muziki yalikua yanaingilia huku na kutokea kule.....najua utakua una jiuliaza kwann nimemuweka wakati alishafariki toka mwaka jana na shukrani nnazozitoa ni za mwaka huu...nimefanya hivi kwasababu ktk miaka yote mwaka huu ndio umekua wa mafanikio sana kwangu na sababu ni mziki ambao huyu ndio mtu aliekua akinipigia kelele sana nifanye sijui kwann sikumsikilizaga natamani angekuepo aone kile alichokua anakitamani aone watanzania na nje ya tanzania walivyonipokea vizuri...R.i.p brother


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...