Kama unakumbukumbu nzuri wakati nafanya tamasha langu la Christmass na
Ngololo niliuliza mtoto atakae cheza vizuri Ngololo na kushinda nimpe
zawadi gani?…na wengi walisema Nimuendeleze kielimu…. Hawa ndio washindi
wetu walioshinda siku ile, ambao siku ya leo niliwapeleka Rasmi katika
Shule ya East Africa International School iliyopo Mikocheni Dar es
salaam ili waanze Masomo yao…Niliona ni vyema kama mtoto yupo shule ya
kawaida nimuhamishe international school ili niweze kumsaidia elimu bora
zaidi…Niushkuru pia uongozi Mzima na wanafunzi wa Shule ya East Africa
International School kwa kuwapokea vizuri.
Simpo,mmoja wa waratibu akiwa
ameongozana,na washindi wa ngololo Dancing
Nikisarimiana na mkuu wa shule bi,Mercy Githirua
Nilipata nafasi ya kuzungmza na
wanafunzi na kuwausia mambo
mbalimbali ya kimaisha....
Ofisin kwa mkuu wa shule tukimalizia
taratibu za kuwaandikisha shule watoto
Niliongozana na wazazi wao pia
Wakipitia form za usajiri