Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha, Mwigulu Nchemba, ambaye jana alikuwa
miongozi mwa manaibu waziri walioapishwa na Rais Jakaya Kikwete kushika
nyadhifa zao amewaambia watu wanaoponda uteuzi wake kuwa hana haja ya
kubishana nao kwani hawamjui.
Katika maelezo yake, Mwigulu alisema anamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kumwamini kuwa anaweza kumsaidia katika kusimamaia sera na mipango ya fedha nchini. Watu wasionifahamu wanadai mimi sina viwango vya kufanya kazi hii; naomba wafahamu kuwa mimi ni msomi mwenye shahada ya ya pili ya uchumi na hivi sasa niko katika masomo ya kupata shahada ya uzamivu.

Mwigulu aliendelea kusema “Kabla sijaingia kwenye siasa nilikuwa
nafanya kazi katika Benki Kuu ya Tanzania kama mchumi. Ninakwenda Wizara
ya Fedha kusimamia mambo manne ambayo ni uadilifu, ushirikiano,
jitihada na huduma madhubuti ambazo zitatolewa kwa wakati mwafaka.”