Taarifa
iliyotufikia muda huu inasema malori zaidi ya 40 yamezuia njia
kufuatia tukio la kutekwa kwa madereva wenzao watatu wa malori na
majambazi kisha kukatwa mapanga,na inasemekana baada ya tukio hilo
kutokea polisi walichelewa kufika eneo la tukio.
Mbali
na malori kuna mabus ya abiria na magari binafsi ambayo nayo hayawezi
kupita kufuatia agizo la madereva hao ambalo wamesema hawaachii njia
mpaka Mkuu wa Mkoa wa Tabora au Rpc afike,huku wakidai hilo limekua ni
tatizo sugu eneo hilo kutokana na kutokea vitendo vya utekaji mara kwa
mara.
Eneo
hili linaitwa laziba lipo katikati ya mji wa Laziba na Nzega,ni
kilomita 20 kutoka Nzega Mjini,madereva hao wa malori wameziba njia
tangu saa 3 asubuhi hii,japo taarifa inasema tukio la kutekwa kwa
madereva hao limetokea jana saa 3 usiku.