MTANGAZAJI nyota wa miondoko ya taarab Gea Habib wa Clouds FM amejifungua mtoto wa kiume jana jijini Dar es Salaam katika hospitali ya Kinondoni (Kwa Dr Mvungi) kwa njia ya upasuaji na sasa anaendelea vizuri yeye na mtoto wake.
Huyu anakuwa ni mtoto wa tatu kwa Gea ambaye pia husikika katika kipindi cha Leo Tena kinachosikika kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa, akitamba zaidi katika kipengele cha “Heka heka” kinachochimbua live mikasa na vituko vinavyoibuka mitaani.
Akiongea na Saluti5, Gea mke wa Mr Habib, alisema wapenzi wake watamkosa hewani kwa miezi kadhaa kabla ya kurejea tena kazini. Mtangazaji huyu alichukua likizo ya uzazi wiki mbili zilizopita.
Kipindi chake cha taarab cha kila Jumapili saa 12 jioni hadi 3 usiku kinachojulikana kwa jina la “Kwa raha zetu” kilimfanya Gea awe mmoja wa watangazaji mabingwa wa miondoko ya taarab.
Mtangazaji mwenzake katika kipindi cha Leo Tena, Dina Marios, naye pia yuko likizo ya uzazi akitarajiwa kujifungua siku za karibuni.
CHANZO SALUTI 5