Stori: CHANDE ABDALLAH NA DENIS MTIMA, Mwanza
Ama kweli dunia haina huruma! Dada Happy amejikuta akiishiwa nguvu na kuanguka mbele ya kadamnasi na kuzimia pasipo msaada wowote ambapo badala yake watu waliodaiwa kuwa ni vibaka walimuibia vitu vyake vyote.
Kwa
mujibu wa mashuhuda, mrembo huyo ambaye alikuwa katika mishemishe za
kawaida alidondoka ghafla akiwa Mitaa ya Nyakato jijini hapa mbele ya
kituo cha polisi, Januari 4, mwaka huu.
Ilidaiwa kuwa baada ya kupoteza fahamu, wahuni walimliza simu pamoja na fedha zote kisha kumwacha akiwa hana msaada wowote.
Hata
hivyo, dada huyo alisaidiwa na wasamaria wema ambao walimpeleka
Hospitali ya Buzuruga ambapo alipatiwa matibabu na baadaye ndugu zake
walipata taarifa kutoka kwa mashuhuda wanaomjua Happy kisha wakaenda
kumchukua.
Gazeti hili lilitaka kujua kilichompata mrembo huyo lakini madaktari hospitalini hapo walidai hawawezi kutoa siri ya mgonjwa huku ndugu nao wakiweka ngumu kusema kilichosababisha Happy kudondoka ghafla na kupoteza fahamu.
“Mimi
sijui kilichompata lakini sasa hivi hali ni mbaya. Unaweza ukashangaa
mtu kasimama halafu akadondoka ghafla na kupoteza maisha. Cha msingi
tucheki afya zetu mara kwa mara,” alisema mmoja wa ndugu hao ambaye
hakutaka kutajwa gazetini.