Jana
mitandao ya kijamii ilijazwa taarifa kwamba jana jioni, John Mnyika (Mb)
alimwandikia barua ya kujiuzulu Katibu Mkuu wa CHADEMA.
Ofisa
Habari Mwandamizi wa CHADEMA, Tumaini Makene (0752 691569) alijibu kwa
kukanusha kuhusu taarifa hizo na kuongeza kuwa kwa muda uliotajwa, Mhe.
Mnyika alikuwa katika shughuli za chama akitimiza majukumu yake.
Akasema
taarifa hizo ni mradi wa kutengeneza uongo unaofadhiliwa na watu kwa
sababu ya, “kuwasumbua wanachama na Watanzania, lakini pia kutaka
kuonesha kuwa kundi la wasaliti na wanafiki ndani ya chama linaungwa
mkono na watu makini ndani ya chama ambao kama wangekuwa upande wao,
wangesaidia kundi hilo kuondoa taswira hasi linalopata mbele ya jamii.
Wanatafuta uhalali walioupoteza kwa kufanya harakati za kusaliti
mapambano.
Mioyoni
mwao wanaumia kweli kweli kuonekana wanaungwa mkono na watu wasio
wanachama wa CHADEMA, ambao wengine wanalazimika kwenda kuwanunua pale
feri Posta na Kariakoo ili waje kuwashangilia Mahakamani na kukimbia
barabarani.SOMA ZAIDI