Stori: Issa Mnally na Dustan Shekidele, Morogoro
OPARESHENI Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers si mchezo! Safari
hii imenasa tukio la mchumba wa mtu aliyetajwa kwa jina moja la Jose
kuuza mwili.
Za mwizi 40: Mchumba wa mtu baada ya kunaswa na OFM akijiuza licha ya kuaga kuwa anakwenda kwa bibi yake.
Tukio hilo lilijiri eneo maarufu la Baa ya Kaumba iliyopo katikati ya
mji kwenye Mtaa wa Makongoro, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo OFM na
polisi walikuwa kwenye oparesheni za kufichua uovu wa biashara haramu
ya ngono.
OFM NOMA: Mchumba wa mtu na wenzake wakiwa mikononi mwa OFM na Polisi.
Kwa mujibu wa mchumba huyo katika mahojiano na OFM, aliaga kwao
Kilosa kuwa anakwenda Morogoro mjini kumuuguza bibi yake ambaye ni
mgonjwa.
Tofauti na matarajio ya familia yake, mrembo huyo alikwenda kukita
kambi maeneo hayo akijihusisha na biashara hiyo haramu eti kwa madai ya
kusaka fedha ya kununulia sare za harusi yake ambayo inatarajiwa
kufanyika Februari 15, mwaka huu.
Mshangao: Mchumba wa mtu akishangaa baada ya kubambwa na OFM.
Jumatano iliyopita, OFM ilipokea simu kutoka kwa dada mmoja ambaye
alieleza kuwa kuna ‘shori’ ambaye ni mchumba wa mtu anajiuza katika
viunga vya Kaumba.
Dada huyo aliendelea kueleza kuwa yeye ni mmoja wa wajumbe katika
kikao cha harusi ya dada huyo huku akiwa ameshachangia shilingi elfu 50
lakini alishangaa kumuona maeneo hayo hatarishi.
Twendeni: Mchumba wa mtu akiongoza wenzake wanaoshuka kutoka kwenye difenda kuelekea kituoni.
“Niamini mimi, tunakaa naye Mji Mpya (Morogoro). Hata fedha za
advance ya ukumbi, vinywaji, MC na muziki tumeshalipa na harusi yake
inatarajiwa kufanyika Februari 15, mwaka huu.
Baada ya kunyetishiwa habari hizo, kikosi kazi cha OFM kiliingia mzigoni kwa kushirikiana na dada huyo ambaye alivalishwa ‘beji’ yao na kufanikisha kunaswa kwa mchumba huyo.
Baada ya kunyetishiwa habari hizo, kikosi kazi cha OFM kiliingia mzigoni kwa kushirikiana na dada huyo ambaye alivalishwa ‘beji’ yao na kufanikisha kunaswa kwa mchumba huyo.
Chini ya ulinzi: Mchumba wa mtu na wenzake wakiwa chini ya ulinzi kituoni.
OFM ikishirikiana na polisi wanaojua kujituma kwenye majukumu yao
walimtia mbaroni dada huyo akiwa katika pilikapilika zake za kunasa
wanaume huku mmoja wa vijana wa OFM akijifanya mteja na kupatana naye
bei ya kuingia chumbani kwa ‘shoti taimu’.
Baada ya kunaswa, mwanadada huyo alikiri mbele ya OFM kuwa ni bibi harusi mtarajiwa.
“Jamani… jamani ni kweli mimi ni mchumba wa mtu, shetani ameniponza nisameheni,” alisema.
“Jamani… jamani ni kweli mimi ni mchumba wa mtu, shetani ameniponza nisameheni,” alisema.
Hata hivyo, kilio chake kiligeuka cha samaki kwani hakikusikika, yeye
na wenzake walionaswa walipelekwa moja kwa moja katika kituo kikuu cha
polisi ili kupisha sheria ichukue mkondo wake.