SANDRA AFUNGUKA: BONGO MOVIES WANAPENDA RUSHWA YA NGONO!!!

Sandra, staa wa bongo movies amefunguka kuwa tasnia ya filamu ya bongo movies haina faida kwani rushwa ya ngono inadhaminiwa kuliko jambo jingine.
Salma Salmin aliendelea kusema kuwa kikubwa kinachoikwamisha tasnia hiyo ambayo kwa sasa inaongozwa na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ ni watu kusaidiana wenyewe kwa wenyewe kwa kuwa labda wanatoka kimapenzi au kutegemea kupewa rushwa ya ngono ili impe shavu mtu.

Bongo movies si mara ya kwanza kuanikwa kuwa rushwa ya ngono imekidhiri, matukio kadhaa ikiwemo madirector wakinasuliwa live katika fuska ya ngono imeshawahi kuanikwa, ya mwisho ni lile tukio la director aliponasuliwa akila uroda na mke wa watu

“Namsihi sana huyu kiongozi wetu wa sasa awe makini na hili suala, yeye pamoja na utawala wake wote wapinge haya mambo na tushikamane ile kuleta maendeleo, maana kila siku wanaopewa madili ya maana ni walewale lakini wengine tunaheshimika kwa majina tu huku dhiki zikitutawala,” alisema Sandra.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...