WANANCHI
wenye hasira wa Kijiji cha Kisiwa Kata ya Kiloka Wilaya ya Morogoro
Vijini jana usiku wamewauwa kisha kuwachoma moto watu watu
wanaosadikiwa kuwa majambazi.
Akizungumza
na Mtandao huu shuhuda wa tukio hilo Bw Shabani Mango alisema majambazi
hao walivunja nyumba ya mkazi mmoja wa kijijini hicho na kuiba shilingi
490,000.
"Jamaa walifka hapa majira ya saa 8 usiku wakiwa na pikipiki Feko yenye namba za usajiri T310
BTC wakipakizana mshikaki,walivunga geni na kuingia ndani ambapo
walipora kiasi hicho cha fedha "alisema Mango na kuongeza" Fedha hizo
Mwalimu Said Swale Tajiri alizikopa jana mchana kwenye saccos ya Moboto
kwa lengo la kumlipia ada mdogo wake anayesoma jijini Dar es salaam leo
ijumaa alipanga kwenda Dar kulipa ada nahisi jamaa walipata taarifa
kwamba Ticha ana mzigo ndani"alisema Bw Mango.
Akihojiwa
na mtndao huu afisa mmoja wa jeshi la polisi alithibitissha kutokea kwa
tukio hilo na kuwataja majambazi hao kuwa ni Emmanuel Mlapoli na Kessy
Benno ambaye ni boda boda naye pack Pangawe jeshini.
CREDIT: MATUKIO NA MICHAPO BLO