Dodoma. Suala la posho limezidi kuwa kaa la
moto katika vikao vya Bunge la Katiba vinavyoendelea mjini Dodoma leo,
hali iliyomlazimu mwenyekiti wa muda, Pandu Ameir Kificho ateue timu
maalum ya watu 6 kutazama jinsi ya kuboresha viwango vya posho hizo.
Timu hiyo inatarajiwa kuyachunguza kwa undani
mahitaji ya wajumbe wa Katiba, kisha kuisaidia serikali kutafuta jinsi
ya kuongeza posho hizo.
Wajumbe wa timu ya posho ni pamoja na mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Uratibu na Bunge), William Lukuvi.
Wengine ni mjumbe wa asasi zisizo za kiserikali
Paul Kimiti, Mbunge wa Peramiho Jenister Mhagama (CCM) na wajumbe wa
Baraza la Wawakilishi Asha Bakari na Mohamed Aboud Mohamed.