Mchezo
wa Ligi ya Mbaingwa barani Ulaya uliopigwa jana kati ya Arsenal ya
England dhidi ya mabingwa watetezi, Bayern Munich ya Ujerumani katika
dimba la Emirates jijini London, uligubikwa na kila aina ya vituko
ambavyo kuna baadhi ya mashabiki wanadai kuwa ni sehemu ya mchezo na
wengine wakidai siyo uungwana.Sahau kuhusu kadi nyekundu ya mlinda
mlango wa Arsenal Wojciech Szczesny ambaye anadaiwa pia kuonesha alama
zisizofaa ambazo huenda akaadhibiwa na UEFA.
Pia
sahau kuhusu Mesut Ozil na David Alaba kukosa penalti kwa kila timu,
jambo kubwa lililoibuka sasa ni Robben kudaiwa kumtemea mate Sagna
ambaye alikuwa amelala chini wakati wa mchezo huo.
Watu
mbali mbali hasa mashabiki wa soka duniani kote ambao wanatumia mtandao
wa mawasiliano ya kijamii wa Twitter wameeleza hisia zao baada ya
kuiona video ambayo inamuonesha winga wa Bayern Munich Robben akiwa
amemuinamia mlinzi wa Arsenal Bacary Sagna na kumtemea mate kwenye
nywele.
Arjen Robben akionekana kumtemea mate Bacary Sagna mgongoni
Wengi
wa walioiona video hiyo wamekuwa wakidai kuwa ni kweli Roben alimtemea
mate Sagna huku wengine wakisema kuwa ni jasho lililomtoka na siyo
mate.