Kamanda
wa kanda maalum ya Dar es salaam Kamishina Suleman Kova akizungumza
na wanahabari muda huu ofisini kwake juu ya kufukuzwa kwa askari hao.
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewafukuza kazi kwa fedheha
askari wanne wa Jeshi la Polisi kutokana na makosa ya kujihusisha na
vitendo vya uhalifu. Askari waliofukuzwa wanatoka katika vikosi
mbalimbali kama ifuatavyo:
E.6396 CPL RAJABU MKWENDA @ UGORO wa Makao Makuu ya Polisi.
· F.9412 PC SIMON wa Kituo cha Polisi Kati.
· F.9414 PC ALBERNUS KOOSA wa Kikosi cha Bendi ya Polisi D’Salaam
· F.9512 PC SELEMAN wa Kituo cha Polisi Kigamboni
Uchunguzi
wa awali umeonyesha kwamba askari hao wamekuwa wakijihusisha na uhalifu
ikiwa ni pamoja na tukio la tarehe 09/03/2014 eneo la Mbezi Beach “A”
ambapo majambazi wapatao 15 walifika katika ofisi ya Kampuni ya Kichina
ijulikanayo kwa jina la HONG
YANG inayojishughulisha na ujenzi na uselemala.
Katika
tukio hilo majambazi wapatao 11 wakivamia ofisi hiyo majira ya saa
04:30 Asb, na kupora vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja fedha taslim, simu,
n.k. na kutoweka.
SOMA ZAIDI
|
Home » Uncategories » ASKARI WANNE WA JESHI LA POLISI WAFUKUZWA KAZI KWA KWA KUJIHUSISHA NA VITENDO VYA UHALIFU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)