Pamoja na kufana lakini shughuli hiyo ilijaa vimbwanga vya mastaa ambao walidhihirisha kuwa yale wanayoigiza kwenye sinema ndiyo maisha yao halisi wanapokuwa mitaani.
Steve Nyerere akikata keki.
Baadhi ya mastaa wa kike walitia fora kwa kuvaa ‘vinguo’ vya
kihasarahasara vilivyoacha nje sehemu kubwa za maumbile nyeti ya miili
yao.“Duh! Unajua baadhi ya mastaa hawa utadhani hawana wazazi, sijui wanaona kukaa utupu ndiyo ustaa?
“Hebu waangalie wanavyotudhalilisha sisi wanawake wenzao utadhani hawajazaliwa Tanzania, kwa nini wasibadilike?” alihoji mmoja wa mastaa wanaojua thamani yao.
Kwa upande wa mastaa wa kiume, wapo waliolewa kupita maelezo lakini kituko kilikuwa kwa chipukizi ambaye alianguka chini mithili ya papai lililodondoka lenyewe mtini kutokana na kulewa tilalila.
Kwa upande wake, staa wa kike wa sinema, Salma Jabu ‘Nisha’ kwa mara ya kwanza alionekana akiwa amevaa kihasara kwani aliacha ‘nido’ zake nje, jambo ambalo lilizua mjadala midomoni mwa watu wakidai kwamba siyo kawaida yake kwani ni binti wa Kiislamu.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, ‘kaka mkubwa’ katika tasnia hiyo na mmoja wa wanahisa wa Bongo Movie Unity, Vincent Kigosi ‘Ray’ na mpenzi wake, Chuchu Hans waliingia mitini kwa kutotokea katika pati hiyo kiasi cha kuzua maswali kibao.
“Mhh! Hapa kutakuwa na namna, haiwezekani Ray na Chuchu wote waingie mitini,” alisema mmoja wa waigizaji ambaye aliomba hifadhi ya jina.
Mastaa wengine ambao licha ya kupewa mialiko hawakuhudhuria, ni Blandina Chagula ‘Johari’ na Wema Sepetu.
ImeandikWA: SHAKOOR JONGO, IMELDA MTEMA NA GLADNESS MALLYA