SITOI RUSHWA YA NGONO KWA MAMENEJA” MSANII ISABELA AFUNGUKA...!

Staa wa Bongo Fleva, Isabela Mpanda.
STAA wa Bongo Fleva, Isabela Mpanda amewachana wasanii ‘wanaotembea’ na mameneja wao kwani ni ujinga wa mawazo na yeye kamwe hawezi kufanya hivyo.
Akizungumza na Glob hii, Isabela alisema katika maisha yake hajawahi kuwa na uhusiano na meneja au prodyuza na huwa anawashangaa na kuwasikitikia wasanii wanaofanya hivyo wakati siyo njia sahihi ya kujikwamua kimuziki.
“Huwezi kuchanganya kazi na mapenzi, kamwe siwezi kutoka kimapenzi na meneja wangu kwa sababu najua ufanisi wa kazi utakuwa mdogo tu,” alisema Isabela.
Staa Huyo hivi sasa anatamba na wimbo wake unaojulikana kwa jina la TARATIBU”  akimshirikisha Luten Karama, Wimbo huo ameshautolea video yake unaweza kuitazama hapa:


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...