Bunge
Maalum la Katika Limekutana Jioni Hii kuendelea na Shuguli zake Lakini
Mvutano Mkubwa Umejitokeza Hali iliyosababisha Vurugu Kubwa
Iliyoambatana na Kuzomea Zomea,Mvutano Huo Uliibuka Pale Mjumbe Tundu
Lissu Aliposimama kuomba Muongozo Kuhusu Marekebisho ya Kanuni Ambayo
Tundu Lissu anamtuhumu Mwenyekiti wa Bunge Hilo Kupitia Kamati ya
Uongozi kuleta Marekebisho Kinyume cha Kanuni zilizopitishwa na Bunge
Hilo la Katiba.
Mwenyekiti
wa Bunge Hilo Mh Samwel Sitta Aliingilia Kati kujaribu Kutoa Ufafanuzi
Pamoja na Wajumbe Wengine Akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Serikali Lakini
hali ya Kuzomea Iliendelea Ndipo Mwenyekiti wa Bunge Hilo Alipolazimika
Kuliahirisha Bunge Hilo Mpaka Kesho na Kuamuru Mabadiliko hayo Yapelekwe
kwenye Kamati Ya Kanuni
Subscribe to:
Post Comments (Atom)