Shabiki akimtukana David Moyes |
Kichapo
cha bao 3-0 walichopata jana kutoka kwa Manchester City kimewakasirisha
mashabiki wa Manchester United, na wameamua kuelekeza hasira zao kwa
kocha Davidi Moyes na Sir Alex Ferguson.
Kufungwa
huko kulipandisha hasira za mashabiki wa timu hiyo ambapo wale
waliokuwa karibu na David Moyes walilazimika kushikwa na walinzi
wakitaka kumshambulia huku wengine wakielekeza hasira zao kwa Ferguson.
Mashabiki wanalaumu uamuzi wa Ferguson kumwachia mikoba Moyes kama kocha wa Manchester United.