Madereva wa Bajaj wakiwa wamemweka kati dereva bodaboda.
Watu wakitawanyika baada ya muafaka.
MADEREVA wa Bajaj wanaopaki maeneo ya Bamaga-Sinza jijini Dar es Salaam leo walimzingira dereva wa bodaboda na kuzua mzozo baada ya wote kugongana uso kwa uso na kusababisha mizigo iliyokuwa kwenye Bajaj izagae hovyo.
Tukio hilo la aina yake lilichukua nafasi baada ya dereva wa bodaboda kukutana uso kwa uso na dereva Bajaj ambapo wote walikuwa wamevunja sheria ya kupita njia ya watembea kwa miguu lakini dereva wa Bajaj alizua mzozo mkubwa akitaka alipwe na dereva bodaboda wakati wote waliumia.
Kutokana na mzozo huo madereva wa Bajaj walimzingira dereva wa bodaboda huku kukiwa na mvutano, kundi moja likiwa yuue wa Bajaj alipwe lakini lilizidiwa nguvu na kundi la wale waliokataa asilipwe na hivyo yule wa bodaboda kurudishiwa ufunguo wa chombo chake na kuondoka kwa kasi eneo hilo.
(PICHA/HABARI:GLADNESS MALLYA/GPL)