Uchafu!
Picha za madiva wakubwa wa filamu Tanzania, Wema Isaac Sepetu na Aunt
Ezekiel Grayson zimebambwa na gazeti hili hivi karibuni wakiwa katika
hali ya kimalavidavi licha ya kwamba, mmoja ni mke wa mtu, mwingine
mchumba.
Kwa mujibu wa mnyetishaji wetu, ishu hiyo
ilichukua nafasi maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam ambako Wema na
Aunt wamepiga kambi kwa ajili ya filamu yao mpya ya Familia.
Ilidaiwa kuwa, Wema na Aunt ambao kwa sasa
wapo ‘klozdi’ kiasi cha watu kuwa na maswali vipi kuhusu Kajala Masanja,
walipiga picha hizo wakidhamiria kuzifuta baada ya kujiona lakini lililotokea si akili zao, picha hizo zikanaswa na paparazi wetu.
Juzi, Amani liliwatafuta kwa njia ya simu
wawili hao na kuwauliza nini kiliwatia nguvu hadi kupiga picha hizo
ambapo Wema anaonekana akibusu sehemu ya paji la uso la Aunt huku naye
akiwa amelegeza macho kusikilizia.
Wema: “Unajua huyu Aunt ni mtu ambaye
tumezoeana kupita kiasi, tunapomaliza kufanya kazi, tunaanza utani.
Halafu kwetu mbona mabusu ni ishu ya kawaida sana!”
Habari za ndani zinasema, baadhi ya ndugu
wa mume wa Aunt, Sunday Dimonte wamekuwa wakimtumia meseji ‘mista’ huyo
kumweleza uchafu mbalimbali anaofanya mume wake licha ya kutotoa tamko
lolote.
Mbali na Dimonte, baadhi ya watu
waliozungumza na Amani walimtaka Nasibu Abdul ‘Diamond’ kukaa chini na
kufikiri upya kuhusu uamuzi wake wa kumuoa Wema. Wengi wanaamini si
sahihi kwake kwa vile haonekani ‘kutulia’ licha ya kwamba wote
‘hawajatulia’