Wachezaji
wa Yanga wakishangilia bao lililofungwa na Didier Kavumbagu (wa pili
kulia), wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara ilipopambana
na Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Timu hizo
zilitoka sare ya 1-1. bao la Didier Kavumbagu (wa pili kulia) lililopelekea mauti ya Deodatus Lusinde.
SHABIKI
wa Timu ya Yanga SC, Deodatus Isaya Lusinde, mkazi wa Kipunguni A,
amefariki dunia leo baada ya kuanguka ghafla wakati akishangilia bao la
Yanga lililofungwa na Didier Kavumbagu katika dakika ya 14 kipindi cha
kwanza.
Marehemu
amepoteza maisha akiwa chumba cha matibabu mara baada ya kuwekewa
mashine ya oksijeni na taarifa kuhusu kifo cha shabiki huyo
zimethibitishwa na mmoja wa madaktari aliyemhudumia akiwa uwanjani kabla ya mauti kumfika, Nassor Matuzya.
Bwana
Isaya alikuwa Meneja wa Bar ya Rose Hill iliyopo Segerea jijini Dar.
Ameacha mke aitwaye, Rose William Lusinde ambaye ni askari magereza.
Marehemu
amekutwa na mauti hayo wakati wa mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, kati
ya timu yake ya Yanga na Azam, mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.
Mungu ailaze roho ya mwanamichezo, Deodatus Isaya Lusinde mahali pema peponi. AMEN