Ombi la marejeo lililowasilishwa na Katibu
wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda
limetupiliwa mbali na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaamilipotoa uamuzi
wa pingamizi la awali lililowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashitaka
(DPP), akidai kuwa ombi hilo halikuwa na msingi kisheria.
Kesi hiyo iliyosikilizwa kwa saa 1 na dakika 40 ilitolewa uamuzi na Jaji Augustine Mwarija.
Baada ya uamuzi huo, Sheikh Ponda alirudishwa jela huko Segerea jijini Dar akiwa chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi.
Baada ya uamuzi huo, Sheikh Ponda alirudishwa jela huko Segerea jijini Dar akiwa chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi.
(HARUN SANCHAWA NA GABRIEL NG'OSHA/GPL)