OOOH..!MASKINI WASTARA...KWANINI HIVI?!!SOMA ZAIDI HAPA.....!!!

Wastara Juma.
OOOH! Zikiwa zimepita siku chache tangu staa wa filamu Bongo, Wastara Juma kunusurika kifo baada ya kudaiwa kunywa sumu na baadaye kupata ajali, anadaiwa kusumbuliwa na roho wa kifo.

Kupitia ukurasa wake katika Mtandao wa Kijamii wa Instagram, Wastara aliweka picha za wasanii mbalimbali huku akimwelezea kila mmoja alivyo na mwishoni mwa maelezo hayo alimalizia kwa kusema kuwa ameamua kusema kabla hajafa kwani kifo hakiko mbali.
 
Baadhi ya mastaa aliowaelezea ni Tamrina Poshi ‘Amanda’, Denis Swea ‘Dino’, Jacob Steven ‘JB’, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, Halima Yahya ‘Davina’, Riyama Ally, Salma Jabu ‘Nisha’.
Wengine ni Cloud, Lamata, Bondi, Msafiri Kondo na wengineo ambapo baada ya kumuelezea kila mmoja, chini alikuwa akiandika ujumbe huu:
“Sababu ya kufanya hivi, sisi ni binadamu na kifo hakiko mbali, naweza nikafa kabla sijasema lolote kwa watu wangu.”

WASTARA ANASEMAJE?
“Niliandika maneno hayo ili wasanii wote waliowahi kunitendea wema wajue kwamba wao ni watu muhimu sana katika maisha yangu, wapo wengi lakini sikuweza kuwashukuru wote kwa sababu wakati naandika hivyo nilikuwa kwenye hali mbaya sana.

“Unajua siku moja nitakufa maana kifo kiko karibu sana hivyo watakumbuka maneno yangu hayo niliyoandika ya kuwashukuru,” alisema Wastara.
 
Baada ya kuwaelezea kwa kuwaandikia waraka huo, mashabiki mbalimbali waliopo kwenye mtandao huo walionekana kusikitishwa na maneno hayo na kujikuta wakimuuliza maswali yasiyokuwa na majibu kwa wakati huo huku wengine wakidai kuwa Wastara anasumbuliwa na roho wa kifo.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...