Ofisi ya Katibu wa Bunge Maalum
inawatangazia Wajumbe wa Bunge Maalum na umma kwa ujumla kuwa Mkutano wa
Bunge Maalum utaendelea mjini Dodoma leo kwa ratiba ifuatayo:
Tarehe 17/3/201 kuanzia saa 3:00 asubuhi kutakuwa na kiapo kwa Wajumbe wa Bunge Maalum ambao bado hawajaapishwa.
Hivyo Wajumbe wote ambao hawajaapa kiapo
cha ujumbe wa Bunge Maalum wanatangaziwa kufika Idara ya Shughuli za
Bunge Maalum leo saa 2:00 asubuhi bila kukosa kwa ajili ya kutambuliwa.
Saa 11:00 jioni Mwenyekiti wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba atawasilisha Rasimu ya
Katiba kwenye Bunge Maalum.
Tarehe 18/3/2014 kuanzia saa 3:00 asubuhi
Wajumbe wote wa Bunge Maalum watapewa semina kuhusu ufahamu mpana zaidi
wa Kanuni za Bunge Maalum.
Tarehe 19 na 20/3/2014 kuanzia saa 3:00
asubuhi wajumbe wote watapewa semina kuhusu Rasimu ya Katiba ya
Jamhuriya Muungano wa Tanzania.
Tarehe 21/3/2014 saa 3:00 asubuhi kutakuwa
na uteuzi wa Wajumbe wa Kamati za Bunge Maalum na saa 10:00 jioni Mgeni
Rasmi ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atalihutubia
Bunge kuashiria ufunguzi rasmi wa Bunge Maalum Atakaye ipata taarifa hii
amjulishe mwenzake.
Imetolewa na Ofisi ya KATIBU WA BUNGE