Mambo hadharani!
Kigogo ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
anayewagombanisha mastaa wawili Bongo, Jacqueline Wolper Massawe na
Husna Maulid ni huyu hapa. Anaitwa Rajab Mwami Shamweshi.
Staa wa Bongo Muvi, Jacqueline Wolper Masswe.
Habari
zilizolifikia Ijumaa zilidai kwamba baada ya mtafaruku wa mastaa hao
kuripotiwa na gazeti mama la hili, Uwazi la Jumanne iliyopita, jamaa
huyo aliibuka na kuanza kulalamika kwa watu wake wa karibu kuwa
anachafuliwa mitandaoni kwa sababu ya mastaa hao.
PATCHOU MWAMBA NDANI
Ilidaiwa kuwa Mwami alichukizwa na ishu hiyo kwani ilimhusisha mwanamuziki wa FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ ambaye pia ni mwigizaji, Patchou Mwamba ‘Tajiri’ kuwa ndiye humkuwadia kwa mastaa.
Ilidaiwa kuwa Mwami alichukizwa na ishu hiyo kwani ilimhusisha mwanamuziki wa FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ ambaye pia ni mwigizaji, Patchou Mwamba ‘Tajiri’ kuwa ndiye humkuwadia kwa mastaa.
TUANZE NA PATCHOU
Kabla ya kumpata Mwami mwenyewe, Ijumaa lilizungumza na Patchou uso kwa uso amba alifunguka anachokijua juu ya sakata la Wolper na Husna kumgombea mwanaume huyo.
Kabla ya kumpata Mwami mwenyewe, Ijumaa lilizungumza na Patchou uso kwa uso amba alifunguka anachokijua juu ya sakata la Wolper na Husna kumgombea mwanaume huyo.
Alisema: “Mimi nashangaa kuona nachafuliwa mitandaoni lakini ukweli anayefanya hivyo ni Husna.
“Huyo Husna ni kweli aliwahi kutoka na Mwami lakini baadaye alimdharau Mwami kwa sababu alimuona hana pesa.
“Huyo Husna ni kweli aliwahi kutoka na Mwami lakini baadaye alimdharau Mwami kwa sababu alimuona hana pesa.
Mlimbwende Husna Maulid.
“Baada
ya kuona pesa zimemtembelea Mwami akataka kurudi ndipo akakuta jamaa
ameshajiweka kwa Wolper. Hapo ndipo Husna akaanza kuchanganyikiwa.”
Patchou aliendelea kuweka wazi kwamba yeye na Mwami ni mtu na rafiki
yake na pia ni ‘mapatna’ kwenye biashara.
Alisema
amekuwa akikutana naye mara kwa mara Nairobi, Kenya na ndiye aliyemleta
Bongo kwa ajili ya kuanzisha kampuni ya michezo ambapo alifikia
hotelini.
KUWADI?
Alitiririka kwamba hajawahi kumkuwadia mwanamke lakini anachojua Mwami ni anajuana vizuri na
Wolper kwani alimtambulisha walipokutana Nairobi hivi karibuni ndipo akaujua uhusiano wao.
Alitiririka kwamba hajawahi kumkuwadia mwanamke lakini anachojua Mwami ni anajuana vizuri na
Wolper kwani alimtambulisha walipokutana Nairobi hivi karibuni ndipo akaujua uhusiano wao.
Patchou: “Nilishangaa kwa sababu baada ya Mwami kutua tu Bongo, wasichana wa mjini walipojua
ndipo wakaanza kumsaka hadi chumba alichofikia hotelini.“Wengine walidiriki hata kumtumia picha za utupu ili kuwa naye kimapenzi baada ya kupata namba yake.”
ndipo wakaanza kumsaka hadi chumba alichofikia hotelini.“Wengine walidiriki hata kumtumia picha za utupu ili kuwa naye kimapenzi baada ya kupata namba yake.”
Patchou
alisisitiza kuwa yeye si kuwadi kama wanavyomtangaza kwani hata huyo
Wolper alishtukia amekutana naye Nairobi wakiwa na Mwami kwani kabla ya
hapo alikuwa hajuichochote.
Baada ya kumaliza kutoa utetezi wake, aliombwa kumpigia simu Mwami na kumuweka loud speaker
(sauti ya juu) ambapo alimweleza Mwami kila kitu ndipo akakubali kuzungumza na wanahabari wetu akiwa London, Uingereza.
(sauti ya juu) ambapo alimweleza Mwami kila kitu ndipo akakubali kuzungumza na wanahabari wetu akiwa London, Uingereza.
KIGOGO AFUNGUKA
Akizungumzia sakata hilo, Mwami ambaye anadaiwa kuwa na ‘mihela’ hivyo kujitwalia taito ya ukigogo alisema kuwa anamfahamu Husna kama mtu wa kawaida ambaye aliwahi kufahamiana naye.
Akizungumzia sakata hilo, Mwami ambaye anadaiwa kuwa na ‘mihela’ hivyo kujitwalia taito ya ukigogo alisema kuwa anamfahamu Husna kama mtu wa kawaida ambaye aliwahi kufahamiana naye.
KUHUSU WOLPER
Kwa upande wa Wolper alisema kuwa anamfahamu kwa kumsikia na kumuona lakini si kimapenzi kama wanavyomchafulia jina.
Kwa upande wa Wolper alisema kuwa anamfahamu kwa kumsikia na kumuona lakini si kimapenzi kama wanavyomchafulia jina.
“Nilipokuja
Tanzania kwa mara ya kwanza nilifikia hotelini…(anaitaja), kama
wanavyodai hata chumba ndicho chenyewe lakini sikuja kwa ajili ya
starehe za kimapenzi na wanawake, nilikuja kwa biashara zangu, nashangaa
kuona nawekwa mitandaoni hovyo na anayeniweka namfahamu.
“Naomba nisizungumze sana, niishie hapo nikirudi Tanzania nitaongea nanyi kwa uwazi kabisa,” alisema Mwami.
FUMANIZI
Wolper na Husna ambao waliwahi kuwa mashosti walianza manenomaneno hivi karibuni ambapo awali haikujulikana chanzo hadi pale Husna alipoamua kulifungukia hilo la mwanaume.
Wolper na Husna ambao waliwahi kuwa mashosti walianza manenomaneno hivi karibuni ambapo awali haikujulikana chanzo hadi pale Husna alipoamua kulifungukia hilo la mwanaume.
Ijumaa
lilifanya jitihada za kumsaka Wolper kupitia simu yake ya mkononi,
alipopatikana alisema angefika ofisini kwetu kutoa ufafanuzi lakini
mpaka gazeti linakwenda mtamboni alikuwa hajafika na alipotumiwa sms ya
kuulizwa kama angefika au la hakujibu.
>>GPL