Uwanja wa ndege wa Changi wa
Singapore umeibuka kinara na kubeba kwa mara ya pili tuzo ya uwanja bora
zaidi wa ndege duniani kati ya viwanja 410 vilivyopigiwa kura na
wasafiri zaidi ya milioni 12 na laki 8.
Kwa mujibu wa tovuti maalum ya tuzo hizo zilitolewa jijini Barcelona, Hispania. Mwaka jana uwanja huo ulishinda tuzo hiyo pia.
“Kushinda tuzo hii ya thamani kwa
mara ya pili inaonesha kuwa Changi inaonesha kuwa ni zaidi ya uwanja wa
ndege.” Amesema Edward Plaisted, CEO wa shirika la Skytrax la Singapore.
Tuzo hiyo hutolewa kwa kukusanya kura
za wasafiri wa nchi 110 duniani kote na huzingatia ubora wa uwanja na
huduma zinazotolewa kwa wasafiri.
Hiii ni orodha ya viwanja vya ndege kumi bora zaidi kwa mujibu wa tuzo hizo:
- Singapore Changi Airport
- Incheon International Airport
- Munich Airport
- Hong Kong International Airport
- Amsterdam Schiphol Airport
- Tokyo International Airport Haneda
- Beijing Capital International Airport
- Zurich Airport
- Vancouver International Airport
- London Heathrow Airport