Ulinzi ulinzi mkali uliimalishwa mahakamani hapo
MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya imewahukumu kifungo cha miaka 30 kila
mmoja aliyekuwa askari wa Jeshi la Polisi na wenzie wanne wakituhumiwa
kwa unyang’anyi wa kutumia silaha.
Akisoma
hukumu hiyo mahakamani hapo Hakimu mfawidhi wa Mahakama hiyo, Michael
Mteite alisema watuhumiwa wote kwa pamoja wanatiwa hatiani kutokana na
ushahidi uliotolewa na mashahidi wawili.
Alisema
ushahidi uliotolewa na shahidi wa kwanza ambaye alikuwa dereva Ezekia
Matatira (34) na shahidi wa pili Sreedhar Pasupelet(38) mwenye asili ya
Kiasia kwamba haukuacha shaka yoyote na ulishabihiana.
Awali
Mwendesha mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa akisaidiwa na Basilius
Namkambe alisema washtakiwa wote kwa pamoja wanatuhumiwa kwa kosa moja
la unyang’anyi wa kutumia Silaha kinyume cha Sheria kifungu cha 287 sura
ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Mulisa aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Mshitakiwa namba moja ambaye ni Askari Polisi PC James mwenye namba F8302,
Elinanzi
Mshana(22)Mkazi wa Iyela Jijini Mbeya, Askari Magereza mwenye namba B
500 Sajenti Juma Mussa(37) wa Gereza la Ruanda Mbeya,Mbaruku Hamis(29)
Mkazi wa Iyela na Amri Kihenya(38) Mkazi wa Iyela.
Alisema
watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Januari 3, Mwaka huu majira ya saa
11 jioni katika eneo la Mlima Kawetere barabara ya Mbeya Chunya.
Alisema
watuhumiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo kwa kulizuia gari aina ya
Pick Up lililokuwa likiendeshwa na Ezekia Matatira (34) Mkazi wa Iyunga
Jijini Mbeya ambaye alikuwa na mtu aliyekuwa akifahamika kwa jina la
Sreedhar Pasupelet(38) mwenye asili ya Kiasia wakitumia magari madogo
mawili ambayo ni GX 100 Toyota Cresta T 782 BEU na Gari lingine ambalo
lilikuwa na namba za Chesesi GX 6011832 aina ya Grand Mark II.
Kwa
upande wake Wakili wa utetezi, Ladilaus Lwekaza, aliiomba mahakama
kuwapunguzia hukumu washtakiwa kwa kile alichodai watuhumiwa bado ni
vijana na hawana rekodi ya makosa ya nyuma.
Aliongeza
kuwa washtakiwa wote kwa pamoja wanafamilia zao ambazo zinawategemea
hivyo wapewe adhabu ndogo ili waweze kuzitumikia familia zao pamoja na
taifa kwa ujumla.
Kutokana
na maombi hayo Hakimu Mteite hakukubaliana naye na badala yake alisema
kwa mojibu wa sheria kutokana na kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha
washtakiwa walipaswa kwenda jela miaka 30 pamoja na viboko.
Aliongeza
kuwa adhabu ya viboko ameifuta kutokana na mshtakiwa namba mbili
kujeruhiwa kwa risasi wakati wa tukio hivyo watasamehewa wote kwa pamoja
ila watatumikia kifungo cha miaka 30 jela kila mmoja.
Mwisho.
Na Mbeya yetu
|