Aliyekua
Mwenyekiti wa tume ya taifa ya kukusanya maoni ya katiba Mheshimiwa
Jaji Joseph Sinde Warioba leo kupitia kipindi cha dakika 45 cha ITV
amezungumza mambo mengi sana ya msingi kuhusu muungano yakiwemo yale
yanayoihusu Tanzania bara na Tanzania visiwani,haya ni miongoni mwa
mambo hayo.
1.Mchakato
umeanza nadhani kwa kusuasua bunge limechukua muda mrefu kutengeneza
kanuni na wameanza haikua mwanzo mzuri mpaka imefika mahali wamefarakana
lakini tunaendelea na mchakato bado matumaini yapo.
2.Sisi
tulipoenda kufanya kazi tulienda kukusanya maoni ya Wananchi tulichukua
maoni ya Wananchi kwa ujumla tukapeleka mapendekezo ambayo tuliamini ni
ya kuwaunganisha Wananchi tulichotegemea ni kwamba Bunge nalo
lingekwenda na muelekeo huo lakini toka mwanzo likaonekana bunge
limejiunda katika makundi badala ya kuanagalia suala lenyewe la maoni ya
Wananchi likaanza kuonekana mgawanyiko toka mwanzo wanatengeneza
kanuni.
3.Wakati
tunakabidhi rasimu ya kwanza nilisema ili tuendelee na muungano
inahitaji ukarabati mkubwa na tukasema kwa tathmini ya tume itakua ni
vigumu sana kufanya ukarabati huo ndiyo maana tumependekeza serikali
tatu.
4.Tulipopita
kwa wananchi walikua wanauzungumzia muungano walisema tuuboreshe
muungano lakini wakati wote wakasema tatizo letu ni muundo wengi
walizungumzia muundo tulionao,tulianza kuorodhesha mambo yote
yaliyosemwa na bara na visiwani.
5.Zanzibar
wamekwenda wamepitisha sheria wanasema sheria zozote zitakazotungwa na
Bunge la Muungano haziwezi kutumika Zanzibar mpaka zipelekwe kwenye
Baraza la Wawakilishi maana yake Baraza la wawakilishi limekua kubwa
kuliko Bunge la Muungano.
6.Tuna
mahakama ya rufaa ina madaraka nchi nzima wameenda wametunga wamebadili
katiba yao wamesema kuna mambo fulani fulani haki za
binadamu,mashauriano yanayotoka kwenye mahakama za kazi na kutafsiri
katiba ya Zanziba hayo hayatakuwa kwenye madaraka ya muungano lakini
kwenye katiba ya muungano imesema katiba hii ina mamlaka yote.
7.Tusiingize
jeshi kwenye mambo ya siasa za makundi Jeshi ni la nchi,mimi
nimetumikia nchi hii nimekua kwenye utumishi wa umma kwa muda mrefu
mpaka nikawa Waziri Mkuu na nilipokuwa Waziri Mkuu nilikua nazunguka
nchini kuangalia shughuli za kimaendeleo na kila nilipoenda kama kuna
kambi ya jeshi karibu nilikua naenda kukaa nao.