Hii ni
stori nyingine tena ya 2014 ambayo inaingia kwenye list ya zile stori
ambazo ukishaisoma au kuipata unaanza kufikiria mara mbilimbili na
kujaribu pia kutengeneza picha yako mwenyewe kama upo eneo la tukio.Watu
wa karibu wa Mtuhumiwa huyu walijitokeza Mahakamani ili kuangalia kama
ndugu yao aitwae Simon Ngozi (21) ataweza kupata dhamana kwenye kesi
inayomkabili ya kubaka mtoto wa miaka tisa.Imetokea Kenya ambapo jamaa
alikua amepelekwa Mahakamani Makadara Nairobi lakini ghafla akamshangaza
kila mtu baada ya kutaka kumaka Mwanamke aliekua karibu yake baada ya
kuanza kumshikashika.
Mshukiwa
huyu alikuwa kortini kujibu tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka tisa April
2014 ambapo wakati anataka kumbaka Mwanamke huyu Mahakamani tena kwenye
eneo la wazi, alimpiga mtama kwanza Mwanamke huyo lakini kwenye
purukushani zake hakufanikiwa manake Polisi walimuwahi.
Shughuli
za Mahakama zilisimama kwa muda baada ya tukio hilo kutokea ambapo baada
ya hapo Mwanamke alietaka kubakwa alisema ‘nilikua nimeketi karibu naye
na mara ya kwanza alilishika begi langu nikalisogeza mbali nikidhani ni
mwizi lakini bila aibu akanishikashika tumboni kabla ya kunisukuma
nikaanguka sakafuni
Baada ya
hapo dada wa mtuhumiwa alimuomba mwanamke huyo kumsamehe ndugu yake
akisema yuko katika hali hiyo baada ya mchumba wake kumtoroka kwa sababu
ya kesi ya ubakaji.
Hili
linakua tukio jingine mimi kulisikia mwaka 2014 la kituko Mahakamani
baada ya mawili ya Mwanza ambapo moja ni Mahabusu kujipaka kinyesi na
kujaribu kutoroka akidhani hiyo mbinu itasaidia mtu asimshike, mwingine
ni alievua nguo zote kushinikiza atendewe haki kwa kisa cha mauji
alichobambikiwa.
Kituko
kingine ambacho kilivunja rekodi kabisa ni cha Wafanyakazi wawili wa
Mahakama nchini Italia kufanya Hakimu kuahirisha kesi baada ya wawili
hao kuonekana wakifanya mapenzi kwenye chumba cha pili pembeni ya chumba
kilichokua kinaendeshewa kesi