KITENDO cha Manchester United kukosa tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa
Ulaya kutaipa hasara timu hiyo ya Pauni Milioni 30, imeelezwa na
Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ed Woodward.
Pamoja na hayo, Woodward
amesema kwamba haitaiathiri k;abu hiyo katika solo la usajili. "Kutokana
na mikataba ya Televisheni, tunakadiria tutakosa Pauni Milioni 30 za
michuano ya Ulaya. Matarajio ya klabu yalikuwa ni kurejea kwenye Ligi ya
Mabingwa naa utaona kwenye usajili wetu,".
Hasara:
Mwenyekiti wa Manchester United, Ed Woodward (katikati) amesema klabu
itakosa Pauni Milioni 30 kwa kutoshiriki michuano ya Ulaya
Mazungumzo: Giwji wa United, Ryan Giggs alipigwa picha nchini Uholanzi akiwa na kikao na Van Gaal Jumatano
Akizungumza
katika mkutano wa simu, alisema: "Katika msimu wa 2013-14, tumemaliza
vibaya katika nafasi tab saba, ambayo inamaanisha hatutashiriki michuano
ya Ulaya.
"Kuwa na uhakika kila mmoja katika klabu anapambana
kuhakikisha msimu ujao tunakuwa katika kiwango cha juu cha Manchester
United.
"Tumefanya mabadiliko ya bench la Ufundi Aprili, tumefurahi
kuwa na Ryan Giggs kwa kumalizia msimu vizuri. Kwa sasa tunaelekeza
nguvu zetu katika kupata kocha mpya na tarajia atatangazwa muda si
mrefu,".
Louis van Gaal ndiye kocha anayetarajiwa kuichukua
Manchester United baada ya Fainali za Kombe la Dunia atakapoiongoza kwa
mara ya mwisho Uholanzi.
Jumatano Giggs alitua Uholanzi na akapigwa picha na inasemakana alikwenda kufanya mazungumzo na Van Gaal kwa niaba ya klabu.
Home » Uncategories » MAN UNITED: TUMEPATA BONGE LA HASARA KWA KUVURUNDA...ILA SASA TUTASAJILI TIMU LA KUFA MTU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)