Home »
Uncategories »
NJEMBA ‘AWAVUA’ NGUO WEMA, AUNT EZEKIEL
NJEMBA ‘AWAVUA’ NGUO WEMA, AUNT EZEKIEL
Unknown
8:58 AM
Stori: Mwandishi wetu
Mastaa wawili wa Filamu za Kibongo, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel
walikipata cha moto walipokuwa kwenye msiba wa Adam Kuambiana, Bunju nje
kidogo ya Jiji la Dar, baada ya kutukanwa na njemba mmoja aliyekuwa
amelewa.
Mastaa wawili wa Filamu za Kibongo, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel wakiwa katika Msiba wa Adam Kuambiana.
Sakata hilo lilijiri usiku mwingi wakati mastaa hao walipokuwa
wameenda kulala kwenya matanga ambayo yalihudhuriwa na mastaa kibao,
nyumbani kwa mke wa marehemu
Mwanaume mmoja (jina lake
halikupatikana) alianza kumtukana Wema kuwa hana uzuri wowote kama
walivyokuwa wakimuona kwenye runinga.
Kitendo cha njemba huyo, kilimkera Wema na kuanza kujibishana naye, Aunt akaununua ugomvi na kujikuta naye akitemewa mbofumbofu.
Hata hivyo, mwisho wa sakata hilo Wema na Aunt waliamua kunyamaza
kwani walibaini kuwa walikuwa wakijibishana na mtu ambaye ‘network’ yake
ilikuwa bize kwa gambe.