Baada ya msemaji wa kambi ya
Upinzani Bungeni ambaye ni waziri kivuli wa wizara ya
Habari,Michezo, Vijana na utamaduni kumtuhumu Zitto Kabwe
kuhusika na kinachoitwa ufisadi katika shirika la TANAPA na
NSSF, mashirika haya yameamua kutoa ufafanuzi kuhusiana na
tuhuma hizi ili kuweka mambo sawa..
.
Meneja
Uhusiano wa TANAPA, Paschal Shelutete ameliambia gazeti la
Mwananchi toleo la leo ( May 30) kuwa shirika hilo
linakitambua kiasi hicho kilichotajwa na wapinzani na kwamba
fedha hizo zilikuwa ni malipo ya wasanii wa Leka Dutigite
ambao walifanya kazi ya kuitangaza Hifadhi ya Saadan...
“Leka
Dutigite ilifika Hifadhi ya Saadan na kuitangaza kupitia kazi za
sanaa... sikumbuki ni lini lakini walifanya kazi na DvD zake zipo.
“Ifahamike si Leka Dutigite pekee, tunafanya kazi na wasanii mbalimbali kutangaza vivutio, mbuga na hifadhi zetu,” Shelutete ameliambia gazeti la Mwananchi
Naye
Meneja Kiongozi wa Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa NSSF,
Eunice Chiume ameliambia gazeti hilo kuwa pesa walizozitoa kwa kundi
hilo zilikuwa malipo ya kutengenezea wimbo maalumu wa shirika hilo na
nyingine ni za udhamini wa onyesho lililofanyika mwaka jana mkoani
Tanga.
“Kweli
mara ya kwanza tuliwalipa Sh25 milioni wasanii wa kundi hilo ili
watutengenezee wimbo na Sh56 milioni zilikuwa za udhamini wa onyesho
lao, lakini kwa masharti ya kututangaza jambo ambalo lilikuwa na
mafanikio kwetu kwani tumefanikiwa kupata wateja wapya 30,000 kutoka
sekta isiyo rasmi,” alisema Chiume.
Alisisitiza
kuwa wametumia kiwango hicho cha pesa ili kujitangaza kwa kuwa hata
mashirika ya kijamii yanapaswa kufanya hivyo ili kuvutia wateja wengi
zaidi.