Watu
wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Kiislamu wameshambulia kituo cha polisi
na mahoteli na vijiji mjini Mpeketoni, pwani ya Kenya .
Makabiliano
makali yameripotiwa sehemu kubwa ya Jumapili usiku huku wakaazi
wakitorokea maeneo ya msitu karibu na kisiwa cha Lamu..
Shirika
la msalaba mwekundu linasema kuwa hadi kufikia sasa watu 48 wanahofiwa
kuuawa kartika shambulizi hilo lililotokea usiku wa kuamkia leo.
Hata hivyo vyombo vya habari vinasema idadi hiyo huenda ikawa juu zaidi.
Shambulizi
lilifanyika usiku wa kuamkia leo watu waliokuwa wamejifunika nyuso zao
wakiwa wamejihami vikali walivamia vituop vya polisi , hoteli na benki.
Shambulizi hilo linakuja siku kadhaa baada ya serikali ya Uingereza kufunga ofisi zake kwa hofu ya usalama.
Duru za jeshi la Kenya zimearifu kuwa wapiganaji hao hawajajitambulisha ni wa kundi gani.
Baadhi ya
walioshuhudia wamearifu BBC kuwa wameona maiti kadhaa na majeruhi wengi
japo Polisi hawajathibitisha ni watu wangapi wameuawa.
Kenya
imekumbwa na mashambulio kadhaa kutoka kwa wapiganaji wa kisomali wa Al
Shabaab tangu ipeleke wanajeshi wake ndani ya Somalia mwaka wa 2011.
Duru
kutoka kisiwa cha Lamu zimearifu kuwa wapiganaji hao walifika katika
malori mawili na kurusha kifaa kama bomu ndani ya kituo cha polisi kisha
wakavamia na kuiba silaha.
'Washambuliaji ni kina nani ?'
Msemaji
wa Jeshi la Kenya Meja Emmanuel Chirchir ameandika katika mtandao wa
Twitter kusema kuwa wapiganaji hao wameshambulia kijiji kimoja na
kufyatua risasi kiholela katika kituo kikuu cha biashara.
''Huenda wapiaganji hao wakawa Al shabaab,'' ameongeza Major Chirhir.
Usiku
wote ndege za polisi zimepaa eneo la Mpeketoni hadi Lamu kudadisi hali
ilivyo huku polisi wakikabiliana vikali ardhini. Kamanda mkuu wa kaunti
ya Lamu ameondoka na maafisa zaidi wa polisi kusaidia makabiliano
yanayoendelea huko.
Mmoja wa
walioshuhudia amesema kuwa mahoteli yameshambuliwa. "baadhi ya mahoteli
yamewashwa moto hatujui watu wangapi wamejeruhiwa kufikia sasa.
Tumeambiwa wameshatoroka lakini polisi wanawafuata waliko,'' ameongeza.
'Kivutio cha watalii'
Kisiwa
cha Lamu kilichoko karibu sana na eneo hilo ni maarufu sana kwa shughuli
za kitalii katika eneo hilo la Afrika, huku likiwa na majengo ya kale
zaidi na kihistoria ambayo yameorodheshwa na shirika la Unesco kama
turathi ya kimataifa.Chanzo BBC Swahili