Mwanamume
mmoja katika jimbo la Kano, nchini Nigeria, amepelekwa katika kituo cha
matibabu ya kiakili baada ya kusema kuwa hamwamini Mungu. Taarifa hii
ni kwa mujibu wa shirika moja lisilo la kiserikali nchini Nigeria.
Mubarak
Bala alizuiliwa kinyume na matakwa yake hospitalini baada ya familia
yake kumpeleka huko kwa matibabu. Duru katika hospitali hiyo zimesema
kuwa mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 29 alitibiwa kwa matatizo ya
kiakili na kwamba hataendelea kuzuilikwa kwa muda mrefu.
Jimbo la Kano lina idadi kubwa ya waumini wa kiisilamu, na limekuwa chini ya sheria za kiisilamu tangu mwaka 2000.
Shirika
hilo la kimataifa limesema kuwa wakati ambapo Bala aliwaambia jamaa
wake kuwa hamuamini Mungu, familia yake uilimpekeka kwa daktari kuuliza
ikiwa akili yake iko timamu.
Licha
ya kufahamishwa kuwa mwanamume huyo hana tatizo lolote la kiakili,
familia ya Bala ilitafuta ushauri wa daktari mwingine aliyewafahamisha
kuwa hatua yake ya kumkana Mungu, inatokana na matatizo ya kiakili.
Bwana
Bala, ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu, alilazimishwa kupata ushauri
wa daktari wa kiakili , ingawa alitumia simu kuwasiliana na wanaharakati
wa haki za kibinadamu.
Hospitali
ambako alikuwa ana pokea matibabu ilisema katika taarifa yake kuwa
Bwana Bala hana tatizo lolote la kiakili na kuwa yuko sawa.
Alilazwa hospitalini kwa sababu alihitaji kuchunguwa na daktari, ilisema taarifa ya hospitali hiyo.