MWANAMKE ASALIMISHA SHANGA ZA MAJINI KANISANI,.... ANENA MAZITO


Mwanamke anayefahamika kwa jina la Asnath Terevaeli akikabidhi shanga kwa Mchungaji Kiongozi, (Frank Endrew) wa Kanisa la Ufufuo na Uzima mkoani Arusha.
Mwanamke anayefahamika kwa jina la Asnath Terevaeli akikabidhi shanga kwa Mchungaji Kiongozi, (Frank Endrew) wa Kanisa la Ufufuo na Uzima mkoani Arusha.atika hali ya kushangaza, mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Asnath Terevaeli hivi karibuni aliamua kukabidhi kanisani shanga za majini kwa kile alichodai kuwa, zimekuwa zikimtesa na kumfanya akose amani.Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita katika Kanisa la Ufufuo na Uzima mkoani hapa baada ya moto wa Injili kuwashwa na Mchungaji Kiongozi, Frank Endrew
Akizungumza na Risasi Jumamosi, mmoja wa waumini wanaosali kanisani hapo aliyejitambulisha kwa jina la Yusta John alisema, awali mwanamke huyo alionekana mwenye jambo linalomtatiza na lilipotolewa tangazo la wenye matatizo kupita mbele, Asnath alifanya hivyo huku akiwa ameshika shanga mkononi.
“Watu wengi walikuwa na shauku ya kujua lililomsibu mama huyo lakini alipofika alimkabidhi mchungaji Frank shanga hizo zilizotengenezwa kiasili zinazodaiwa ni za majini.
Shanga zilizosalimishwa.
Shanga zilizosalimishwa.
“Mwenyewe alieleza kuwa, alipewa kama zawadi na mwanaye lakini cha ajabu zimekuwa zikimtesa na kumfanya akose amani.
 Mchungaji Gwajima
Mchungaji Gwajima
 “Alidai kuwa kila alipovaa alihisi mauzauza mwilini hivyo akaona sehemu sahihi ya kujikomboa na mateso hayo ni kanisani,” alisema Yusta.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...