Lori
la kusafirisha mafuta likiwa na shehena kubwa ya mafuta aina ya Diesel
limeteketea kwa moto baada ya kupata ajali ya kugongwa na lori lingine
katika eneo la igurusi wilayani mbarali.
Ajali
hiyo imetokea ikihusisha lori lenye namba za usajili t 417 ABF, mali
ya kampuni ya Camel oil ambalo lilikuwa likisafirisha lita 35,000 za
mafuta aina ya diesel kutoka jijini Dar es salaam kwenda nchini Congo
DRC ambalo linadaiwa kugongwa na lori lingine.
Baadhi
ya wananchi ambao wameshuhudia ajali hiyo wameitaka serikali
kuwalazimisha wamiliki wa malori kuhakikisha magari yao yanakuwa na
madereva wa akiba kwa kuwa wanaamini kuwa ajali hiyo imesababishwa na
dereva wa lori moja wapo kusinzia wakati akiendesha gari kutokana na
uchovu wa safari ndefu.
Mpaka
napata hizi habari hizi na chanzo kinatoka katika hilo la ajali, bado
lori hilo lilikuwa likiendelea kuteketea huku kukiwa hakuna msaada
wowote wa kuuzima moto huo.